IQNA

Jitihada

Darsa za Qur’ani Tukufu zaendelea  Gaza licha ya mashambulizi ya Israel

21:19 - January 07, 2024
Habari ID: 3478163
IQNA - Licha ya mashambulizi ya mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza ambayo yamepelekea watu ya 23,000 kupoteza maisha na malaki kuyahama makazi yao, mafunzo ya Qur'ani Tukufu yanaendelea katika eneo hilo lililozingirwa.

Katika mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza karibu na mpaka na Misri, familia zilijenga mahema ambamo watoto hujifunza Qur’ani Tukufu pamoja na mafundisho na maadili ya Kiislamu.

Hema moja limejengwa katika shule katika kitongoji cha al-Janina, ambapo watu wengi waliokimbia makazi yao kutoka kaskazini mwa Gaza wanaishi.

Sheikh Mahmoud, mmoja wa wanaofundisha Qur'ani hapo, alisema hatua hiyo inalenga kuwaongezea ari watoto na kuwatia moyo kujifunza Qur’ani Tukufu.

Aliongeza kuwa walimu ni wanafunzi wa vyuo vikuu vya Kiislamu ambao wamejitolea kwenda kwenye mahema na kufundisha Qur’ani.

Utawala katili wa Israel umefyatua zaidi ya tani 65,000 za makombora na mabomu kwenye Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7, 2023, na kuua takriban watu 22,300, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Utawala ghasibu wa Israel ulianzisha vita dhidi ya Gaza ili kukabiliana na operesheni ya Okotoba 7  ya harakati za wapigania ukombozi wa Palestina au wanamuqawama ambao walikuwa wakilipiza kisasi jinai za zaidi ya miaka 75 za utawala huo katili.

3486713

Habari zinazohusiana
captcha